Salum Bausi kocha mpya Mwenge FC...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
TIMU ya soka ya Mwenge FC umemuita kocha Salum Bausi kwenda kuinoa timu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba.
Kocha Salum Bausi
Bausi ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes mwaka 2013 ameitwa kikosini humo kwa lengo la kushirikiana na kocha aliyekuwepo Salum Bajaka katika mashindano ya kombe la Mapinduzi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu wa timu hiyo Gongo Shaaban Gongo amesema kuwa tayari kocha huyo ameshawasili kisiwani Pemba na kuanza mazoezi na timu hiyo kwa ushirikiano mkubwa na Bajaka.
Amesema ujio wa kocha huyo unawapa matumaini makubwa ya kuwa timu yao itaweza kufanya vyema katika mashindano ya Mapinduzi Cup yanayoanza leo.
“Ujio wa kocha huyu ni kusaidiana na makocha waliopo sasa, ili kuitengeneza Mwenge ili iwe tishio kwa vilabu vya Zanzibar,” amesema Gongo.
Mwenge ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 25.




No comments:
Post a Comment