Serikali yapiga marufuku matumizi fedha za kigeni...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI imesema wakati inaandaa mchakato wa mabadiliko ya
sheria ya matumizi ya fedha za kigeni nchini, imepiga marufuku ununuzi na uuzaji kwa kutumia fedha hizo kuanzia
Januari mosi, 2018.
Waziri wa fedha na mipango Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
mwenendo wa hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka
2017/18.
“Suala la matumizi ya fedha za kigeni sambamba na shilingi ya
Tanzania nchini, linasimamiwa na (a) sheria ya usimamizi wa fedha za
kigeni ya mwaka 1992 (Tha Foreign Exchange Act, 1992, (b) Sheria ya Benki Kuu
ya Tanzania ya mwaka 2016 na (c) Tamko la serikali la mwaka 2007 kuhusu
matumizi ya fedha za kigeni kulipia bidhaa na huduma katika soko la ndani,”
“Matumizi haya wakati wa kufanya miamala mbalimbali yanaweza kuwa
na athari kiuchumi ikiwa ni pamoja na kudhoofisha thamani ya shilingi na sheria
iliyopo kwa sasa inasisistiza kuwa sarafu ya Tanzania ndiyo fedha halali na mtu au
taasisi yoyote itakayokataa kupokea malipo kwa shilingi ya Tanzania
atachukuliwa hatua za kisheria,” amesema.
Kufuatia hatua hiyo Dk. Mpango ametoa maagizo matano
yanayotakiwa kizingatiwa kuanzia Januari 1, 2017, maagizo hayo ni bei zote hapa
nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizo zitajumuisha kodi ya
nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, vyombo vya
usafiri na vifaa vya kielekroniki.
Mengine ni bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au
wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa
kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni.
Bei hizo zitajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na visa kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi.
Bei hizo zitajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na visa kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi.
Ameongeza kuwa ni viwango vya kubadilisha fedha
vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na
visizidi vile vya nje.
Mengine ni mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia
bidhaa au huduma yoyote hapa nchini kwa fedha za kigeni na vyombo vya dola
viwachukulie hatua kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo hayo ya
serikali.




No comments:
Post a Comment