Twaweza:Fedha zinaongeza chachu walimu kufundisha...soma habari kamili na maatukio360..#share


Na Salha Mohamed , Dar es salaam

UTAFITI  umedhihirisha kuwalipa walimu fedha kunaboresha matokeo ya kujifunza kwa wanafunzi


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa matokeo ya utafiti wa KiuFunza awamu ya pili wa kutoa motisha kwa walimu uliofanyika katika kipindi cha 2015 /2016 katika shule 120 hapa nchini. 



"Utafiti  umedhihirisha kuwa kuwalipa walimu fedha baada ya matokeo ya kujifunza kunaweza kuboresha matokeo ya kujifunza," amesema 

Amesema kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2015 asilimia 31 ya walimu hawakuwepo shuleni kabisa ambapo asilimia 34 walimu hao walikuwepo lakini hakuwepo darasani akifanya shughuli zake zingine na asilimia 35 ilionesha wapo darasani. 

"Kwa mwaka 2016 takwimu zilishuka ambapo asilimia 27 ya walimu hawakuwepo shuleni kabisa, asilimia 32 yupo shuleni lakini hayupo darasani na asilimia 41 wapo darasani, "amesema. 

Amesema kiwango cha kujifunza kipo chini huku idadi ya wanafunzi na mahitaji kuongezeka kuwa ni miongoni mwa changamoto za elimu nchini. 

Amesema utafiti huo umeonesha matokeo mazuri kwa kumpa mwalimu motisha kunampa ari mwalimu kufundisha mwanafunzi na kufaulu zaidi.  

"Kasi ya mtoto kujifunza inaongezeka katika kipindi kifupi unavyomuongezea mwalimu motisha, "amesema. 

Amesema asilimia 91 ya walimu katika utafiti huo wameupenda mpango huo na asilimia 63 ya walimu waliafiki serikali iweke mfumo rasmi wa motisha kwa walimu kutokana na matokeo mazuri. 

Utafiti huo umefanywa na taasisi ya Twaweza kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) pamoja na Shirika la Innovations for Poverty Action (IPA) ambapo takribani sh 266,315 zilitumika kulipa walimu 788 motisha kati ya 900 huku wastani wa sh milioni 3.6 kikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwalimu kupata. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search