Meja Generali Sharif:Haturudi nyuma....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MKUU wa majeshi Zanzibar Meja Generali, Sharif Othman amesema kutokea kwa tukio la kufa kwa wanajeshi nchini Kongo ni mwanzo wa kuongeza nguvu zaidi ya kuimarisha amani nchini humo na kamwe hawatorudi nyuma.
Ametoa msimamo huo leo visiwani Zanzibar katika hafla ya kuaga miili ya wanajeshi hao waliouwawa wiki iliyopita nchini Kongo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kulinda amani katika nchi hiyo.
“Tumepoteza roho za wanajeshi wetu ambao walikuwa tegemeo katika kutekeleza majukumu ya kazi zetu lakini hatutarudi nyuma kupambana hadi tuhahakikishe Congo inakuwa tulivu.
Miili ya wanajeshi tisa walioua nchini Congo iliwasili saa 7:30 mchana na hafla hiyo ilifanyika katika kambi ya Jeshi Migombani mjini Zanzibar, ambapo wanajeshi na wananchi mbali mbali wakiwa na familia za maiti hao walihudhuria.
Amesema vikosi vyake vilioko nchini Congo havitarudi nyuma au kutishika kutokana na tukio hilo, hadi wahakikishe kuwa nchi hiyo inakuwa katika hali ya utulivu.
Katika hafla hiyo pia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliungana na wananchi na wanajeshi hao na kusema kuwa Serikali iimesikitishwa na msiba huo na watahakikisha wanakua bega kwa bega na familia ambazo zimepata msiba huo.
Alisema kuwa pamoja na kuwa ni msiba wao wote lakini aliwaomba ndugu wa marehemu hao kuwa na subra na Serikali bado ipo pamoja na nao katika kipindi chote kigumu cha msiba huo.
‘’Serikali imesikitishwa sana na kushtushwa na vifo hivyop na katika kuhakikisha hilo ndio maana ikatoa waakilishi maalumu kuwakilisha kwenye misiba yote tisa ambao wataiwakilisha Serikali katika familia ambazo zimepata misiba hio’’alifafanua.
Viongozi wengine waliohudhuria katika msiba huo ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed ambae alisema Serikali ya Znzibar imepokea kwa mshtuko mkubwa vifo vya wanajeshi hao waliokuwa wanalinda amani nchini Congo.
Balozi Seif amesema Serikali itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kulinda amani katika bara la Afrika.
Amesema kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa na kila mpenda amani popote alipo.
Waziri asiye na Wizara maalum katika Serikali ya Zanzibar, Said Soud Said amesema ni wakati muafaka kwa nchi kutafakari upya mikataba ya kimataifa.
Mara baada ya kuagwa kwa miili ya wanajeshi hao, kila familia ilikabidhiwa maiti yake kwa ajili ya utaratibu wa maziko ambao ulisimamiwa na wanajeshi kwa kutumia taratibu zote za Kijeshi.
Mungu ametoa na jina lake lihidimiwe na mungu awalaze mahala panapostahiki maiti hao Aamin.
No comments:
Post a Comment