Vanessa Mdee aibuka kivingine ...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MSANII wa muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee amezindua albamu
yake ya kwanza ya ‘Money Mondays’ yenye nyimbo 18.
Vanessa Mdee na Mohombi Moupondo wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albamu ' Money Mondays' jijini Dar es Salaam.
Amezindua album hiyo jana jijini Dar es Salaam na nyota
wa muziki aliyeshinda tuzo ya kimataifa ya Grammy 2016, Mohombi Moupondo raia wa
Sweeden mwanye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC).
Akizungumza katika uzinduzi huo Vanessa amesema kwenye albamu
hiyo ameshirikisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi na inatarajia kuingia
sokoni Januari 15, 2018.
“Katika albamu hii nimeshirikisha nyota kadhaa wa muziki akiwemo
Joh Makini kutoka Tanzania, Caspper Nyovest wa Afrika Kusini, Konshens wa
Jamaica na Mahombi,” amesema Vanessa.
Msanii huyo bora wa kike kwa Afrika Mashariki amesema imani
yake ni kwamba albamu hiyo itafanya
vizuri kwa kuwafikia watu wengi na lengo ni kuzidi kupenya zaidi katika soko la
ndani na nje.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na mastaa mbalimbali ndani na nje
ya nchi uliambatana na Vanessa kuachia nyimbo
chache zilizopo katika albamu hiyo ikiwemo ‘Kwangu Njoo’ aliomshirikisha
Mohombi.
Vanessa amefanya uzinduzi huo baada ya hivi karibuni
kutangaza kusainiwa na lebo ya muziki ya Universal.
Kwa upande wake Mohombi amesema anafurahi kuja kumuunga mkono
Vanessa katika uzinduzi huo na kuongeza kuwa ni mategemeo yake albamu hiyo kufanya
vizuri kulingana na ubora iliyonayo.




No comments:
Post a Comment