WADAU :Ushirikiano unahitajika kudhibiti unyanyasaji....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WANAHARAKATI wa kutetea haki
za wanawake na watoto visiwani Zanzibar wamesema ushirikiano wa pamoja unahitajika katika
kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyofanywa kwa wanawake
na watoto.
Waziri wa afya Zanzibar , Mahmoud Thabit Kombo
Wakizungumza katika kikao
cha kamati cha mradi wa GEWE III kilichokutana ofisi za Chama Cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar iliyopo Tunguu mkoa wa Kusini Unguja
wamesema hatua iliyofikia ni wazi matendo hayo hayatoweza kuondoka iwapo
hakutakuwa na ushirikiano.
Wamesema ushirikiano mdogo unakwamisha kufuatilia kesi za unyanyasaji.
“Mie nadhani cha msingi ni
umoja na ushirikiano tu ndio utakaosaidia kupunguza vitendo vya unyanyasaji kwa watoto na
wanawake. Hii pia itasaidia kufikia malengo tuliyojiwekea”, amesema Sabra
Mwinyinjuma Mgeni ambaye ni afisa Wanawake Wilaya ya Magharibi A .
Amesema katika kupambana na
kesi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinaongezeka kila siku ni lazima wajenge ushirikiano
kwa kila mmoja kujua kuwa ni jukumu lake
katika kupambana na vitendo hivyo.
“Kila jambo linahitaji
umoja, mshikamano na ushirikiano kinyume na hili hatuwezi kufikia kule ambapo
tunakokutaka, tujitahidini kuwa na umoja na ushirikiano,” amesema Fatma Juma
Jabu ambaye ni Mratibu wa Wanawake wa sehiya ya Mwanakwerekwe wilaya ya
Magharibi A Unguja.
Amesema kuna matukio
yanatokea lakini wanashindwa kuyafatilia kutokana kukosa
ushirikiano hasa kwa wazee ambao watoto wao wamefanyiwa vitendo vya
udhalilishaji.
‘’Pamoja na mambo
mengine umefika wakati kwa wazee kupewa
elimu zaidi ili wanapopata tatizo waripoti na baadae watoe ushirikiano na
wasiogope kuona kuwa mambo yao yatakuwa wazi.’’
No comments:
Post a Comment