Takukuru yamkamata mgombea wa CCM...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Singida
TAASISI ya kupambana na
kudhibiti rushwa(TAKUKURU) inamshikilia mshindi wa kura za maoni CCM jimbo la
Singida Kaskazini (kabla ya kufutwa), Haider Gulamali kwa tuhuma za kutoa
rushwa.
Haider Gulamali
Hatua hiyo inafuatia baada
ya jana CCM kufuta mchakato wa kura ya maoni uliofanyika katika jimbo la
Singida kaskazini kutokana na baadhi ya wagombea kujihusisha na vitendo vya
rushwa.
Katibu wa Nec-Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema kutokana na hali hiyo Haider Gulamali na Elia Mlangi wamezuiwa
kugombea nafasi hiyo kutokana na kutuhumiwa kujihusisha na rushwa.
CCM imewataka wote wenye nia
ya kutaka kuteuliwa na chama hicho
kugombea ubunge wachukue fomu kesho Alhamisi na wazirudishe jioni ya siku hiyo. Awali
jumla ya wagombea 17 walijitokeza kuwania nafasi hiyo.
Tayari tume ya uchaguzi
imetangaza uchaguzi wa jimbo hilo na mengine mawili kufanyika Januari 13, 2018.
Kata sita nazo zitashiriki katika uchaguzi huo wa marudio. Majimbo mengine ni
Longido Kaskazini na Songea mjini.
Haider Gulamali ambaye ni mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia mjini Dodoma, aliibuka wa kwanza kwenye kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida Kaskazini kwa kupata asilimia 60.
No comments:
Post a Comment