Watoto 52 wazaliwa mkesha Krismass... soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohamed,Dar es salaam


JUMLA ya watoto 52 wamezaliwa mkesha wa Krismass katika hospitali ya taifa ya rufaa Muhimbili (MNH), Amana na Temeke.


Mwanahamisi  Omar mkazi wa Mbagala akiwaangalia watoto wake mapacha aliojifungua usiku wa kuamkia chrismass,Mwanahamisi alipata rufaa kutoka hospitali ya Zakhem

Akizungumza Dar es Salaam leo na matukio360, Muuguzi Mwandamizi MNH, mariam Mlawa amesema wanawake  sita wamejifungua katika hospitali hiyo. 


Amesema wanawake wawili walijifungua watoto mapacha ambapo mmoja alijifungua kwa upasuaji.


"Wazazi sita walijifungua usiku wa kuamkia leo, wazazi wawili walijifungua kwa upasuaji  na wanne walijifungua kawaida, mzazi mmoja alijifungua mapacha kwa upasuaji,"amesema.


Amesema hakuna tofauti kwa uzazi wa mwaka huu na mwaka jana na kuongeza kuwa wazazi watano walipata rufaa kutoka hospitali zingine huku mmoja akitumia bima ya afya.


"Afya za mama pamoja na watoto hao zinaendelea vizuri,"amesema.


Katika hatua nyingine,Ofisa Muuguzi Kiongozi  hospitali ya Temeke,Rashid Ally amesema katika mkesha wa krismass wamezaliwa watoto 12 ambapo wakike ni watatu na wakiume wakiwa tisa.


"Hakuna upasuaji wala waliojifungua  mapacha  na Afya zao zinaendelea vizuri, "amesema.


Aidha, Muuguzi wa zamu hospitali ya Amana, Agnes Simon amesema waliojifungua ni 32  ambapo watoto wakiume ni 18 na wakike 14 huku wazazi watano walijifungua kwa upasuaji.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search