Baraza la vyama vya siasa wachaguana....soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es
Salaam
BARAZA la vyama vya siasa nchini limefanya uchaguzi wa viongozi wa kamati nne huku kila kamati ikiwa na mwenyekiti na makamu mwenyekiti ambao wataongoza kamati hizo kwa muda wa miaka miwili kwa mujibu wa sheria.
Pia limetoa siku 30 kwa kamati ya sheria na utawala bora ya baraza hilo kuhakikisha inajadili mapendekezo ya sheria na kanuni mpya ya vyama vya saisa kisha kuleta mrejesho.
Pia limetoa siku 30 kwa kamati ya sheria na utawala bora ya baraza hilo kuhakikisha inajadili mapendekezo ya sheria na kanuni mpya ya vyama vya saisa kisha kuleta mrejesho.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Mwenyekiti wa
TADEA John Shibuda akizungumza katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa
uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkwawa ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es salaam
kulia Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti
wa baraza hilo John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao
cha baraza hilo kilichokuwa kimeketi jijini Dar es Salaam
Miongoni mwa viongozi waliochaguliwa ni John Momose Cheyo kutoka chama cha UDP ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na Salum Mwalimu kutoka chama cha Chadema ambaye ni Makamu Mwenyekiti.
Kamati ya bunge na siasa, mwenyekiti ni Juju Martin Danda kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na makamu mwenyekiti ni Mohamed Masoud Rashid kutoka chama cha Chauma.
Kamati ya sheria na utawala bora itaongozwa na mwenyekiti Hassan K. Almas kutoka chama cha NRA na Said Soud kutoka chama cha AFP ambaye ni Makamu Mwenyekiti.
Kamati ya Maadili na Mahusiano ni Mohammed Ali Abdullah kutoka chama cha Demokrasia Makini ambaye ni Mwenyekiti na Peter A. Magwira kutoka chama cha DP ndiye Makamu Mwenyekiti.
Viongozi wa kamati za baraza wamechaguliwa kwa kupigiwa kura ya siri na wajumbe wa kila kamati. Mwenyekiti akitokea upande mmoja wa Tanzania, Makamu Mwenyekiti atatokea Zanzibar.
Wenyeviti wa kamati za Baraza la vyama vya siasa, Mwenyetikiti wa Baraza la vyama vya siasa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa ndio huunda kamati ya Uongozi ya vyama vya siasa.
Kuhusu siku 30, Shibuda amesema “Barazala vyama vya siasa nchini limeazimia kwa kauli moja kuwa mjadala wa mapendekezo ya Sheria na Kanuni mpya ya vyama vya siasa, utaanzia kwenye kamati ya Sheria na utawala bora”, amesema.
Ameongeza “Itajadili mapendekezo tata yaliyokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali na pia kamati
itakuwa na jukumu la kukusanya upya maoni ya mapendekezo ya kutunga sheria na
kanuni mpya ya vyama vya siasa, tumeipa siku 30 kukamilisha kazi hiyo, lakini
ikitaka tuiongeze muda tutafanya hivyo,”.
Shibuda amesema kamati hiyo ikikamilisha kazi yake
italeta mrejesho mbele ya baraza kwa maboresho na wajumbe wakiridhia
yatawasilishwa kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kukamilisha utaratibu wa
utungaji wa Sheria na Kanuni mpya ya vyama vya siasa.
Amesisitiza kuwa
kwa sasa sheria na kanuni za vyama vya siasa zilizopo zitaendelea kutumika hadi
hapo zitakapotungwa sheria mpya.
No comments:
Post a Comment