Chadema wavunja makubaliano ya Ukawa...soma habari kamili na matukio 360...#share

Na mwandishi wetu,Dar es salaam
CHAMA cha Chadema kimebadilisha msimamo wake na sasa kinashiriki uchaguzi wa marudio wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni na Siha utakaofanyika Februari 17,2018

Mwaka jana kwa niaba ya Ukawa, mwenyekiti taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kutoshiriki uchaguzi wowote  mdogo wa marudio hadi hapo NEC itakapokutana na wadau wa vyama vya siasa kujadili na kuondoa kero na vikwazo vilivyojitokeza katika uchaguzi wa udiwani wa kata 43 wa mwezi Novemba,2017


TAARIFA KWA UMMA, KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA KINONDONI NA SIHA.


Kamati Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.

Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1.   Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma.

2.   Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi.

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.

Imetolewa Leo tarehe 19 Januari, 2018.
John Mrema - Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search