Chelsea yamsajili Giroud , ManCity yakwama kumsajili Riyad Mahrez...soma habari kamili na matukio360....#share
Na mashirika ya kimataifa
Chelsea imemsajili mshambuliji wa Arsenal Olivier Giroud kwa mkataba wa miezi 18 utakaogharimu paundi milioni 18.
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31, anaondoka arsenal baada ya kufunga maba 105 katika mechi 253 tangu asajiliwe kutoka klabu ya Ufaransa ya Montpellier kwa kitita cha paundi milioni 12 mnamo mwezi Juni 2012.
Borussia Dortmund pia wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi hadi mwisho wa msimu huu.
Awali Dortmund ilimuuza Pierre-Emerick Aubameyang kwa Arsenal.
Wakati huohuo Manchester City wamejiondoa katika makubaliano ya kumsajili winga wa Leicester Riyad Mahrez wakidai kwamba uhamisho wake ungeigharimu klabu hiyo dau kubwa la paundi milioni 95.
Siku ya Jumanne mchezaji huyo alikuwa amewasilisha ombi la kuondoka katika klabu yake ya Leicester
No comments:
Post a Comment