IGP Sirro amkabili 'nabii' anayeendesha ibada katika baa...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MKUU wa jeshi la polisi, IGP Simon Sirro amefanya mazungumzo na Tito Machija anayejihita nabii ambaye amekuwa
akionekana mitandaoni akifanya mambo yasiyoendana na maadili ya dini na injili
anayodai kuihubiri katika baa.
Hata hivyo inadaiwa baada ya mazungumzo hayo jeshi la polisi mkoani humo lilimkamata kwa mahojiano zaidi
Hata hivyo inadaiwa baada ya mazungumzo hayo jeshi la polisi mkoani humo lilimkamata kwa mahojiano zaidi
IGP Sirro akizungumza na Nabii Tito mjini Dodoma leo.
IGP Sirro amezungumza na ‘mhubiri binafsi’ huyo licha ya jeshi hilo kutotoa taarifa rasmi ya kilichojiri na utaratibu unaoendelea iwapo ni kumhoji au kumfikisha mahakamani.
Nabii huyo ambaye video zake zimekuwa zikisambaa zikihamasisha kuoa mke
zaidi ya mmoja, kufanya ngono na wafanyakazi wa ndani,
anatumia pombe kupata waumini na anadai hataki nyimbo za injili kwenye ‘ibada’
zake, na baadhi at ibada zake hufanyia baa.
Pia ameonekana akicheza nyimbo za bongo fleva akiwa ‘madhabahuni’ badala ya kwaya na huku akieleza kuwa wafadhili wake wanatumia
pombe, hivyo na yeye lazima waumini wake watumie pombe ambazo amezifanyia
upako.
No comments:
Post a Comment