Magufuli amtumbua mkurugenzi wilaya ya Butiama...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


RAIS John Magufuli  ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Solomon Ngiliule kutokana na kutumia fedha kinyume na miongozo iliyowekwa.


Pia katibu mkuu TAMISEMI ametakiwa kumchukulia hatua stahiki mweka hazina aliyehusika kwenye matumizi mabaya ya  fedha  wilayani Butiama

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), selemani Jafo akitangaza utenguzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Solomon Ngiliule

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofanya ziara Mkoani Mara, kubaini watendaji wa halmashauri kushindwa kusimamia vyema maeneo yao ya kazi katika miradi ya maji na afya.


Akitangaza utenguzi huo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amemwelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kumchukulia hatua stahiki mweka hazina aliyehusika wakati wa matumizi mabaya yaliyofanyika ya fedha za serikali.


"Nawataka watendaji wote walio chini ya Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni za Utumishi wa Umma na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa letu, "amesema.


Amesema asilimia 20 ya fedha za bajeti ya serikali imeelekezwa Tamisemi, hivyo wafanye kazi kwa ufanisi na kuzingatia maadili.


"Niwasihi wakurugenzi wengine wote ambao wamepewa dhamana na Rais, tunawapima kwa utendaji wao wa kazi...na wale ambao watabainika hawawndani na kasi hii ya sasa lakini kipaumbele chetu ni kuhakikisha thamani ya fedha na suala la kujali utu na uwajibikaji katika meneo yao ya kazi ni jambo la msingi, "amesema.


Jafo amefafanua kuwa dhamana waliopewa wakuu wa Idara, wakurugenzi ni kubwa hivyo wahakikishe wanafanya kazi zao kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.


Amesema kila mtu anapaswa kuhakikisha anafanya kazi kwa maslahi ya wananchi na si ya binafsi.


Ameongeza kuwa,  hadi sasa serikali inafanya uchunguzi na kwamba watakaobainika kuhusika katika utumiaji mbovu wa fedha hawatasita kuwachukulia hatua.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search