Jaji mkuu: Tutawahoji, kuwachukulia hatua wote wanaoingilia uhuru wa mahakama....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es salaam
MAHAKAMA nchini imesema inatarajia kuunda kamati ya maadili
kama ya Bunge itakayokuwa na uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwa wote watakaoingilia
uhuru wa mhimili huo wa nchi
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya wiki ya sheria itakayoaanza Januari 27 hadi Januari 30, 2018.
Pia imesema majaji na mahakimu ndiyo wenye wajibu na jukumu la kuhakikisha wanalinda uhuru wa mhimili huo na kwamba wanatakiwa kuwaita wanaouingilia,
kuwahoji na kuwachukulia hatua inapobidi.
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Jaji mkuu, Profesa Ibrahimu Juma
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya maadhimisho ya
wiki ya sheria nchini yanayotarajia kufanyika viwanja vya mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam.
“Inatakiwa ifike mahali kufanya kama Bunge, kuunda kamati ya
maadili itikayo wawajibisha wanaoingilia muhimili huu, mfano mtu anapolikosea Bunge anaitwa kwenye kamati na kuhojiwa, lakini niwatake Mahakimu na Majaji wasiruhusu mtu yeyote kuingilia uhuru wa mahakama,” amesema jaji mkuu Prof. Juma.
Amesema sababu ya mihimili kuingiliana ni kutokana na
kutokufuatwa kwa kanuni, taratibu na katiba ya nchi na kuwa ili
kuondoa hali hiyo kila mhimili unatakiwa kufuata mamlaka iliyopewa .
“Ninawakumbusha wananchi na viongozi mbali mbali nje ya mahakama
kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania mamlaka ya utoaji haki ni ya mahakama tu,
na nawasihi viongozi wote wa serikali wenye mamlaka ya kikatiba na kisheria
wabaki ndani maeneneo yao ya kikatiba na wajiepushe kuingilia maneo yaliyo
ndani ya haki, hadhi na mamlaka kikatiba ya maahakama,” amesema
Akizungumzia kuhusu wiki ya sheria, amesema siku ya sheria
itakuwa Februari 1, 2018 na ni siku maalum ambayo itaashira kuanza kwa shughuli
za mahakama kwa mwaka huu.
Hivyo kabla ya siku hiyo mahakama pamoja na wadau muhimu
katika sekta ya sheria watatumia siku tano kuanzia Januari 27 hadi Januari 30,
2018 kutoa elimu ya sheria kwa wananchi watakaopata nafasi ya kuhudhuria na
hiyo itakuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya sheria.
Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma amesema kilele cha maadhimisho
hayo itakuwa Februari 1, 2018 katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa
Chimala jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.
No comments:
Post a Comment