Jaji mfawidhi Beatrice Mutungi awaonya watumishi wa mahakama...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Beatrice Mutungi amewataka watumishi wa mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na kusiwepo na kero za rushwa, utoro kazini ama kutowajibika ipasavyo.
Pia amesema hatarajii kuona wananchi wanasubiri mwezi mzima kupata nakala za hukumu kama ilivyokuwa mwanzo na upotevu wa majalada ya kesi kwa sababu mahakama nyingi nchini sasa zina sehemu za kuhifadhi.
Jaji Beatrice Mutungi aliyesimama
Mutungi ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Kawe lenye ukubwa wa mita za mraba 1020 likiwa na kumbi ndogo mbili za mahakama ofisi za watumishi, mahakimu pamoja na mahabusu kwa wanaume, wanawake na watoto.
Amesema uzuri wa jengo hilo uendane na kasi ya usikilizwaji wa kesi na utoaji wa haki kwa wakati.
Naye Khamadu Kitunzi ambaye no Mhandisi ujenzi wa Mahakama ya Tanzania amesema ujenzi wa jengo hilo umeghalimu jumla ya Sh 552,952,567.00.
Amesema ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya utafiti wa ujenzi wa majengo ya mahakama kwa kutumia teknolojia ya gharama nafuu ya Moladi na kuwa na miundombinu imara.
Kitunzi amesema ujenzi huo ulianza Julai 2016, lakini siku halisi za ujenzi pa
Kitunzi amesema ujenzi huo ulianza Julai 2016, lakini siku halisi za ujenzi pa
hadi jengo kukamilika ukiondoa miundombinu nyingine ni siku 90.
"Kwa kuwa utafiti ulikuwa ukiendelea mara kwa mara ujenzi ulisimama kupisha uchambuzi, majadiliano na maamuzi kufanyika," amesema
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment