Watanzania kufika idadi ya watu milioni 59.4 mwaka 2021...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
INAKADILIWA hadi kufikia mwaka 2021 idadi ya watanzania itafikia watu milioni 59.4 na kwamba kila mwaka kunaongezeko la watu milioni 1.6.
Ongezeko la vijana na watoto ni asilimia 50. Na ifikapo mwaka 2030 Tanzania itakuwa na watu milioni 77.9
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akimkabidhi Profesa Malline Mbonile taarifa ya makisio ya idadi ya watu Tanzania baada ya kuizindua leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua taarifa ya makisio ya idadi ya watu Tanzania na kwamba kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu hasa kwa watoto na vijana inaleta changamoto.
"Asilimia 50 ya watu wote ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18. Na hii ni changamoto,"amesema.
Amesema asilimia kubwa ya watoto kwenye nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko ya kidemografia kutoka kiwango vya juu vya vifo huku viwango vya uzazi vikiwa juu.
Dk. Mpango amesema asilimia kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yeyote duniani kwa kuwa kundi hilo linahitaji mahitaji ya pekee ambayo lazima yatimizwe na serikali.
"Mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na idadi kubwa ya watoto, "amesema na kufafanua kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi kiumri ni asilimia 92 ikilinganisha na wastani wa asilimia 40 kwa nchi zinazoendelea.
Ameongeza ili kukabiliana na changamoto hizo ya serikali imewekeza kwenye elimu kuhakikisha kila mtoto hasa wa kike anapata fursa sawa ya kusoma na kubaki shule.
Amewataka wadau wa ndani na nje ya nchi kutumia takwimu hizo na kutoa onyo kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo bila kushirikisha ofisi ya Taifa ya Takwimu, ni kosa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu Na: 9 ya mwaka 2015.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu Tanzania (UNFPA), Jacqueline Mahona amesema takwimu hizo ni muhimu kote duniani na takwimu sahihi ni nguzo muhimu katika uhakika wa kufanya mipango ya maendeleo.
"Kwa mujibu wa takwimu zilizopo Tanzania ina idadi kubwa ya vijana... Umri kati ya miaka 17 ni asilimia 44 ya idadi ya watu ya watu wenye umri wa miaka 15,"amesema.
Amesema makundi hayo ya vijana na watoto wakipewa nafasi wanauwezo na nguvu za kuchangia katika maendeleo ya nchi ambapo yatakiwa kwa kuwekeza kwenye maeneo muhimu katika ukuaji wao hasa wa kike ili waweze kujitambua na kufahamu wajibu wao kwa jamii na nchi hadi kufikia utu uzima.
"Kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani na Tanzania linatulazimu sisi sote kuongeza juhudi katika kuwekeza huduma za jamii hasa afya na elimu, "amesema.
Amesema ukuaji wa polepole wa idadi ya watu utatoa fursa familia na serikali kuwekeza zaidi katika maendeleo ya watu na kuiwezesha rasilimali watu kuzalisha kwa tija.

No comments:
Post a Comment