Kenya kurusha setilaiti yake anga za juu..soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
NCHI ya Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.
Setilaiti
Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.
Setilaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.
Inasemekana setilaiti hiyo ni ya umbo la mchemraba na ina ukubwa wa sentimita 10 mraba
Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini ni Wakenya wenyewe walioitengeneza.
Setilaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizunguka dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.
Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa sita barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.
Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.
No comments:
Post a Comment