Maandalizi tamasha la busara bambam....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraha Ntambara, Dar es Salaam 

MAANDALIZI ya tamasha la Sauti za Busara,  linalotarajia kufanyika Februari 8, 2018   katika mji Mkongwe, visiwani Zanzibar  yanaendelea vizuri.
Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara Yusuf Mahmoud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Februari 8 hadi Februari 11, 2018 lenye kauli mbiu ya “kuunganishwa na Muziki”, Waafrika na wageni kutoka katika kila pembe ya dunia.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema tamasha linaitangaza Zanzibar na Tanzania sehemu mbali mbali duniani kwa kuwa linavutia mapromota wa kimataifa na kutoa fursa adhimu kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuupeleka mziki wao duniani kote.

“Ndani ya majukwaa matatu kwa siku nne, tamasha litakuwa na maonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa asilimia 100 yatapigwa mbashara. Tamasha litawaweka pamoja wanamuziki wadogo na wakubwa kutoka katika viunga vyetu na hata nje ya nchi, likibeba dhumuni moja huku tukisimama pamoja kupitia kauli mbiu ya ‘kuunganishwa na  muziki”, amesema Yusuf.

Yusuf amesema orodha ya wanamuziki imejitosheleza katika nyanja nyingi

Watakao hudhuria tamasha hilo watashuhudia kuzaliwa upya  kwa mwanamuziki wa kitanzania, Saida Karoli amabaye alirudi katika tasnia ya muziki mwaka jana.


Ametaja baadhi ya wanamuki wanaotarajia kukonga nyoyo za watazamaji katika tamasha hilo la 15 la sauti za busara ni pamoja na Zakes Bantwini (Afrika Kusini), Kasai Allstars (DRC), Somi (Uganda/USA), Ribab Fusion (Morocco), Kidum na tha boda boda band (Burundi/Kenya), Mlimani Park Orchestra (Tanzani), Grace Matata (Tanzania) na Msafiri Zawose (Tanzania).

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search