Kocha mpya Simba asema miezi miwili tu mtaona mambo yangu...soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
KLABU ya Simba leo imemtambulisha kocha mpya Mfaransa Pierre
Lechantre na wa viungo Mtunisia Aymen Habib. Kocha huyo amesema kikosi chake kitaeleweka baada ya miezi miwili.
Kocha mpya wa Simba Pierre Lechantre (katikati) akiwa ameshika jezzi ya simba (wakwanza kushoto) ni kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah na wa mwisho kulia ni Meneja wa kocha huyo Joe Onegofro jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ambayo
hayakuwekwa wazi, kocha hiyo amesema atakuwepo kwa muda mrefu kwa kuwa klabu ina malengo ya
muda mrefu kwa ajili ya kuwa bora barani Afrika.
“Nipo hapa kwa ajili ya ‘project’ ya muda mrefu ili
kuhakikisha timu inakuwa bora, ninaweza kuwepo hapa kwa miaka mitatu au zaidi,”
amesema Lechantre.
Amewetaka kwa sasa mashabiki na wapenzi wa mpira nchini
kuweka pembeni wasifu wake na waangalie kazi ambayo amekuja kuifanya na kueleza
kuwa mabadiliko katika timu yanaweza kuanza kuonekana baada ya miezi miwili.
Kwa upande wake msemaji wa Simba Haji Manara, amesema kocha
huyo atasaidia pia katika maendeleo ya timu za vijana kwani klabu inamalengo
makubwa.
Pia amewataka mashabiki wasimba kuwa na uvumilivu pale klabu
inapofanya vibaya kwani hakuna anayependa kutokea jambo hilo.
Kaimu rais wa Simba Salim Abdallah akiwa ameshika jezi yenye jina la kocha wa viungo Aymen Habib.
No comments:
Post a Comment