Majaliwa: Maafisa kilimo hawapaswi kukaa ofisini...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji na Wilaya za Mbinga wahakikishe wanaunda
kanda za kilimo na kuwasambaza maafisa kilimo na si wakae ofisini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea
na Watumishi wa Halmashauri ya Mbinga, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya
kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo
na Ofisi ya Waziri Mkuu, imesema ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na
watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
“Mkurugenzi wa TC na DC chuja maafisa
kilimo ulionao na uhakikishe wanabakia watatu tu. Abaki DALDO, mtu wa
horticulture na mthamini, wengine wote wasambaze kwenye kanda ili wasimamie
wakulima wakiwa huko huko. Hili litekelezwe na Mkuu wa Wilaya ulisimamie,”
alisema.
Aliwataka maafisa kilimo wa zao la
kahawa waende vijijini na kufanya sensa ili waweze kubaini wana wakulima
wangapi wanaozalisha kahawa.
“Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue kijiji kina wakulima wangapi wa kahawa, na wana ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi? Hii itaisaidia Serikali ijue inahitaji dawa za aina gani, mbolea kiasi gani na miche mingapi kwa wakulima wake,” alisema.
“Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue kijiji kina wakulima wangapi wa kahawa, na wana ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi? Hii itaisaidia Serikali ijue inahitaji dawa za aina gani, mbolea kiasi gani na miche mingapi kwa wakulima wake,” alisema.
“Ninataka hizi takwimu ziwe
zimekamilika ifikapo tarehe 28 Februari, mwaka huu,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka maafisa ushirika wa wilaya hiyo wakasimamie uundwaji wa AMCOS mpya na kuimarisha zile za zamani ambazo zinafanya kazi vizuri.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka maafisa ushirika wa wilaya hiyo wakasimamie uundwaji wa AMCOS mpya na kuimarisha zile za zamani ambazo zinafanya kazi vizuri.
“Maafisa ushirika ninataka nipate
takwimu ya AMCOS very strong (ambazo ziko imara) kwenye wilaya yako. Iifikapo
tarehe 28 Febriari, takwimu hizi ziwe zimekamilika. Kama kuna AMCOS nzuri
ziimarisheni, itisha uchaguzi ili uanze na uongozi mpya,” alisisitiza.
Aliwaeleza watumishi na madiwani
kwamba Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kurudisha heshima ya zao hilo
ambapo zamani iliweza kusomesha watoto kadhaa kwenda sekondari kutokana na
mfuko wa kahawa.
“Zamani zao la kahawa lilikuwa
likisomesha watoto wa wakulima, sasa hivi hakuna hata anayefaidika na zao hili.
Tunataka zao hili liwanufainishe wakulima, iinue uchumi wa wanaMbinga, isomeshe
watoto na iwezeshe wakulima kujenga majumba,” alisema.
Alisema kuanzia msimu ujao wa Mei,
Juni na Julai 2018, ununuzi wa kahawa utafanywa na vyama vya msingi
vinavyotambulika kwa maafisa ushirika.
Aliwaonya watumishi wa Halmashauri
hizo waache kutoa vibali vya ununuzi wa kahawa kwa watu binafsi wanaomiliki
kampuni za kununua kahawa. “Halmashauri ndiyo mnatoa vibali vya kampuni kununua
kahawa. Huu ni mwisho sasa. Hatuna mnunuzi binafsi wala hatuna kampuni binafsi,
hawa wote tukutane kwenye mnada,” alisema.
Alisema hataki kuona watumishi wa
Halmashauri wakionesha vibali vya kununua kahawa kama moja ya chanzo cha mapato
kwenye Halmashauri hizo. “Ni marufuku kuingiza vibali kwenye mapato ya
Halmashauri,” alisema.




No comments:
Post a Comment