Mohamed Salah mchezaji bora Afrika..soma habari kamili na matukio360...#share
Salah alionekana
kuitetea vyema timu yale ya Liverpool mnamo mwaka jana 2017 baada ya
kujipatia goli 23 katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya Uingereza akitokea timu ya AS Roma.
Wapinzani wake nao si
haba kwani Pierre-Emerick Aubameyang, wakati huo huo, alifunga mabao 31 ya
kipekee kati ya michezo 32 katika mashindano yote ya mwisho.
Tuzo hiyo ya shirikisho la
soka barani Afrika ilikuwa na orodha ya wachezaji wapatao 24, miongoni mwa hao
watatu mwezi Desemba Salah, Aubameyang na Mane walitangazwa kuingia katika
hatua ya mwisho ya tatu bora .
Mshindi wa tuzo hiyo kwa
mwaka uliopita alichaguliwa na makocha kwa kushirikiana na manahodha wa timu katika
kila timu ya wanaume barani Afrika.
Sadio Mane kutoka katika
timu ya Liverpool amekuwa mshindi wa pili kwa wingi wa kura, pamoja na
nyota mchezaji wa timu ya Dortmund ,aubameyang kushika nafasi ya tatu kwa wingi
wa kura.
No comments:
Post a Comment