UKAWA waitega NEC uchaguzi Siha, Kinondoni....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
IMEBAINIKA kuwa ushiriki wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge katika jimbo la Kinondoni na Siha ni mtego uliowekwa na UKAWA kwa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC )
Mtego huo ni UKAWA kujiridhisha kama NEC inauwezo wa kuwadhibiti wakuu wa wilaya kutoingilia mchakato mzima wa uchaguzi.
Hashim Rungwe
Katika mahojiano maalum na matukio360, jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama cha Chauma, Hashim Rungwe amesema kilichofanywa na Chadema kinaungwa mkono na Ukawa na kwamba walitangaza kurejea kwenye uchaguzi iwapo malalamiko yao yatashughulikiwa na moja ya lalamiko lilikuwa ni wakuu wa wilaya kuingilia uchaguzi.
Lakini kwa upande wake katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Danda Juju ameshangazwa na uamuzi huo na kwamba msimamo wa mwisho wa vyama vinavyounda Ukawa ni kutoshiriki uchaguzi bado upo pale pale.
Mtego huo ni UKAWA kujiridhisha kama NEC inauwezo wa kuwadhibiti wakuu wa wilaya kutoingilia mchakato mzima wa uchaguzi.
Hashim Rungwe
Katika mahojiano maalum na matukio360, jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama cha Chauma, Hashim Rungwe amesema kilichofanywa na Chadema kinaungwa mkono na Ukawa na kwamba walitangaza kurejea kwenye uchaguzi iwapo malalamiko yao yatashughulikiwa na moja ya lalamiko lilikuwa ni wakuu wa wilaya kuingilia uchaguzi.
"Hivyo katika hili NEC imetuhakikishia kulishughulikia na tayari wamewaandikia barua viongozi hao wa wilaya kuwataka kutojihusisha na uchaguzi.
“Sasa tunataka kuona kama kweli wamerekebisha na hatuwezi kuona kama tupo nje ya mpambano na kama hawajarekebisha tutazidi kulalamika,”amesema
Rungwe amesisitiza walichofanya Chadema ni maamuzi ya Ukawa kwa kuwa wakati wakiteua wawakilishi wa majimbo ya Siha na Kinondoni vyama vingine vilikuwa na uwakilishi walioshiriki kuwapitisha.
Walioteuliwa kugombea katika majimbo hayo ni Salum Mwalimu Juma Kinondoni na Elvis Christopher Mosi jimbo la Siha.
“Najisikia vibaya sana
kuzungumza juu ya suala hili, na kwa bahati mbaya waandishi wa habari wamekuwa wakiniulizia
kuhusu hili, nimekuwa sitaki kulizungumzia na pengine kwako wewe wacha nisema
hivi,”
“Labda kwa ufupi ni
sema kwamba azimio tulilokuwepo nalo la mwisho la vyama vinavyounda Ukawa bado
liko palepale na nilikuwa nazungumza na mwenyekiti wa kamati ya uongozi CUF juu
ya hili, Chadema wamefanya hivyo kama Chadema,” amesema Juju.
Amesema anatarajia
kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif kujadili na kujua
kilichojili na kwamba pia watafanya juhudi za kukutana na Chadema ili
kulijadili suala hilo kwa kina.
Juju amesema wakati Chadema ikisimamisha wagombea
bado yale waliyoyadai na shinikizo waliloweka NEC hadi sasa matokeo yake hayajaonekana.
Amesema kuweka wagombea
siyo vibaya lakini ilitakiwa busara kutumika ili wakutane Ukawa kwa pamoja
wazungumze ili kuwa na mwelekeo wa pamoja
No comments:
Post a Comment