Serikali Equatorial Guinea yanusurika kupinduliwa...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
SERIKALI ya Equatorial Guinea amesema mamluki wametaka kuipindua serikali ya nchi hiyo. Mapinduzi hayo yamezimwa kwa msaada wa idara za usalama za Cameroon
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema
Takriban wanaume 30 waliojihami kutoka Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya kati walikamatwa mwezi uliopita, kulingana na waziri mmoja.
Walipatikana wakiwa na roketi, bunduki na risasi kwenye mpaka nchini Cameroon.
Serikali ya Rais Teodoro Obiang Nguema, imekuwa ikilaumiwa kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.
Wanajeshi nchini Equatorial Guinea walimuua kwa kumpiga risasi mamluki wakati wa makabiliano siku ya Jumatano karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa runinga ya taifa TVGE.
Obiang amekuwa madarakani kwa karibu miaka 40, baada ya kutwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979 na kumuondoa madarakani mjomba wake Francisco Macias Nguema ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.
Katika taarfa iliyosomwa kupitia radio ya taifa, waziri wa ulinzi Nicholas Obama Nchama aliwalaumu mamluki waliokuwa wamepewa kazi na makundi ya upinzani na kusaidiwa na mataifa ambayo hayakutajwa.
Equatorial Guinea imekumbwa na madai ya mapinduzi ya kijeshi siku za awali.
Mwaka 2004 mwanajeshi wa zamani raia wa Uingereza Simon Mann alihusishwa na jaribio la kumpindua Obiang.
Mwanajeshi huyo wa zamani wa Uingereza na mafanyabiashara alikamatwa nchini Zimbabwe mwaka 2004 na kusafirishwa kwenda Equatorial Guinea miaka minne baadaye.
Mwaka 2008, Mann alihukumiwa miaka 34 jela, lakini mwaka mmoja baadaye aliachuliwa baada ya kusamehewa na Obiang.
Equatorial Guinea ni moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu wake wanaishi katika hali ya umaskini.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search