NEC kukutana na wadau vyama vya siasa..soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

TUME ya taifa ya uchaguzi (NEC) kesho  itakutana   na wadau wa vyama vya siasa kujadili mchakato wa uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge na udiwani nchini.




Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (katikati) akifafanua jambo kwenye kikao cha Tume kilichokaa leo (Jumamosi)  Jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Mkuu Mst. wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Katibu wa Kikao hicho ambaye pia  ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan.

Taarifa ya NEC inasema mkutano huo utafanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Nyerere kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.



Wajumbe wa Tume wakipokea na kusikiliza maoni ya Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi mdogo kwenye  moja ya mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Viongozi wa Vyama vya Siasa jijini Dar es salaam.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search