Mawaziri wawili Zimbabwe wafikishwa mahakamani..soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
MAWAZIRI wawili wa zamani wa Zimbabwe wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.
Waziri wa zamani wa Nishati nchini Zimbabwe, Samuel Undenge
Samuel Undenge ambaye alikua waziri wa nishati anatuhumiwa kutumia dola elfu kumi na mbili kwa kampuni ambayo haukufanya lolote.
Kwa upande wa wake Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Robert Mugabe aliyeondolewa madarakani mwezi Novemba, anatuhumiwa kuchangia baadhi ya mali za televisheni ya taifa kwa kanisa moja nchini humo bila ya idhini ya serikali.
Wote wawili wamekana mashitaka hayo.Inatarajiwa kesi hizo zitasikilizwa tena baadae mwezi huu.
Rais mpya Emmerson Mnangagwa ameapa kupambana na rushwa iliyodumu karibia wakati wote wa utawala wa Robert Mugabe.
Lakini wakosoaji wanasema watu wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani ni wale tu wanaohoji namna Mnangagwa alivyoingia madarakani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search