Serikali yasisitiza uwazi shughuli za madini....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
KAMPUNI za madini nchini zimetakiwa kufanya shughuli zake kwa uwazi sambamba na kufuata sheria za nchi ili kuepuka migongano.


Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam Januari 29, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kwenye mkutano wake na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles aliyeambatana na Mshauri masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii kwenye Tasnia ya Uziduaji kutoka Serikali ya Canada, Jeffrey Davidson.

Ujumbe huo ulimtembelea Katibu Mkuu Msanjila kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kwenye Sekta ya Madini ikiwemo suala la Sheria ya Madini, masuala ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) yanayofanywa na kampuni mbalimbali zikiwemo za kutoka nchini Canada na matarajio ya Serikali kwa kampuni (wawekezaji).

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search