Mwenyekiti, katibu wilaya wa Chadema wengine 15 wahamia CCM...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Kilimanjaro
CHAMA cha CCM wilayani Moshi Vijijini kimepokea viongozi 17 kutoka vyama vya upinzani wilayani humo mapema hii leo.

Wamepokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM,Humphrey Polepole akiwa kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu Wilaya ya Moshi Vijijini.



Waliojiunga ni viongozi tisa wa Chadema wakiongozwa na Ekarise Kiwia Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Moshi Vijijini na Emmanuel Mlaki Katibu wa Chadema Wilaya la Moshi Vijijni na katibu wa Jimbo la Vunjo.

Viongozi watano (5) wa NCCR wakiongozwa na Stanley R. Temba Katibu wa NCCR Vunjo pamoja na Viongozi watatu (3) wa TLP wakiongozwa na Kawawa J. Rubega Katibu wa Jimbo la Vunjo

Kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Moshi Vijijini kimewakubalia na kuwapokea ndani ya CCM.

Hii imepelekea Idadi ya Viongozi waliohamia CCM katika ziara ya Polepole Mkoa wa Kilimanjaro kufikia 89.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search