Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne..soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Manchester City inamtaka Aymeric Laporte na inafikiria kutimiza kipengee cha kumruhusu beki wa kati huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 kilichotolewa na Athletic Bilbao cha Pauni milioni 60. (Sun)
Borussia Dortmund inamtaka mshambuliaji raia wa Ufaransa wa timu ya Arsenal Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 31, kama sehemu ya kubadilishana na mchezaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa 28, - au wasitishe mpango huo hadi msimu wa joto. (Mirror)
Olivier Giroud
Chelsea inatafakari kuvunja sera ya kutolipa malipo ya uhamisho kwa wachezaji wake kando na makipa walio na umri wa miaka 30, kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, kutoka Roma. Upande wa Antonio Conte huenda ukakamilisha makubaliano ya mara mbili ya Dzeko na mchezaji wa Roma Italia wa kiungo cha beki kushoto Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 23, kwa thamani ya pauni milioni 44. (Telegraph)
Au Chelsea itawalipia wachezaji wote wawili pauni milioni 50. (Mirror)
Crystal Palace imeanzisha mazungumzo na Inter Milan kuhusu makubaliano ya zaidi ya pauni milioni 8.5 kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele Eder, mwenye umri wa 31. (Mail)
Newcastle ipo tayari kusaini uhamisho wa mkopo wa winga wa Chelsea raia wa Brazil Kenedy, mwenye umri wa miaka 21, katika saa 24 zijazo. (Mail)
Real Madrid inajitayarisha kwa uhamisho wakati wa msimu wa joto wa Mohamed Salah wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 kwa mujibu wa rais wa shirikisho la soka Misri. (Liverpool Echo)
Newcastle inashughulikia makubaliano ya kumleta mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Ufaransa Kevin Gameiro, mwenye umri wa miaka 30, kuingia St James' Park. (Express)
Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 29 yupo nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguuu wake uliovunjika. (Telegraph)
Wasiwasi kuhusu afya ya Fabian Delph unamaanisha kuwa Manchester City inatazamia kumsaini mchezaji wa Shakhtar Donetsk kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 24 Fred hivi sasa, badala ya kusubiri hadi msimu wa joto. (Manchester Evening News)
Winga wa Brazil Lucas Moura, 25, anayelengwa na Tottenham, anasema "hana raha" akiwa Paris St-Germain. (L'Equipe)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe anasema kurudi kwa winga Junior Stanislas, na mshambuliaji wa Norway Joshua King, mwenye umri wa miaka 26, kutoka kuuguza majeraha, ni kama kuwasajili wachezaji wawili. (Bournemouth Echo)

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search