Sumatra kufungia mabasi yatakayochakachua mfumo wa VTS....soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Mbeya

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) mkoani  Mbeya imeanza kufuatilia mienendo ya mabasi ya mikoani na itayafungia ikibaini kuvuruga (kuchakachua)  mfumo wa kuratibu mwendo wa uendeshaji wa mabasi nchini (VTS).

Meneja wa Sumatra mkoani Mbeya, Denis Daudi

Meneja wa Sumatra mkoani Mbeya, Denis Daudi ameiambia matukio360 kuwa mabasi yatakayobainika kuchakachua mfumo huo  hayatotozwa faini na yatafungiwa kutoa huduma ya usafirishaji.

Daudi amesema miaka ya nyuma serikali ilitumia gharama
kubwa za kuvunga vidhibiti mwendo lakini madereva walifanya uharibifu na kuendelea kukiuka sheria za usalama barabarani ikiwamo kuendesha kwa mwendo kasi na kuchangia ajari nyingi.

Amefafanua lengo la serikali kuweka mfumo huo ni kupungua
ajari za barabarani zinazogharimu maisha ya watanzania wengi na kwamba VTS ni maalum kwa kufuatilia mienendo ya madereva kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho.

Daudi amewaonya madereva kutofanya uharibifu katika mfumo na kwamba wazingatie sheria na kanuni mpya zilizowekwa na mamlaka hiyo na si vinginevyo na endapo wakienda kinyume zitawabana.

"Tumetoa elimu elekezi kwa wadau wa usafirishaji  na kanuni mpya zilizowekwa na mamlaka, sasa isitokee tena mkikiuka na kuchukuliwa hatua mkalalamika,"amesema.

Pia ameonya wafanyabishara na waubiri wa dini kutoingia kwenye mabasi kwa lengo la kufanya biashara nakuhubiri  kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria mpya zilizowekwa na mamlaka na endapo watabainika hatua za kisheria zitachukuliwa.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search