Majaliwa amwakilisha JPM mkutano AU Ethiopia....soma habari kamili na matukio360....#share
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye
ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika
Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu,
anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28,
2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa
Addis Ababa, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi
Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia. Januari 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais
wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya
Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais
John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu
cha kumbukumbu, cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa
Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi
huyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu
yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano
huo. Januari 28, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment