Waziri Palamagamba: Wananchi tafuteni suluhu nje ya mahakama....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewashauri wananchi kuhakikisha wanajaribu kutafuta usuluhishi nje ya mahakama kwa matatizo yanayowezekana na ikishindikana ndiyo wapeleke mahakamani.
Ametoa ushauri huo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua jengo la Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni iliyogharimu zaidi ya Sh milioni 594.
Waziri wa katiba na sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akizindua jengo jipya na la kisasa la mahakama ya wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam leo
Kabudi akizindua jengo hilo leo amesema mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana ilikuwa kuwa wanahitaji Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 na kwamba wanauhitaji mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini.
Ameipongeza Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonyesha kwa kufanya utafiti wa kutumia Moladi kwa ujenzi wenye ubora, imara na gharama nafuu.
"Pamoja na mambo mengine tafuteni viwanja zaidi ili jitihada za kuongeza mahakama wilayani Kigamboni ziongezeke kwa kuwa Kigamboni inakuwa kwa kasi," amesema Kabudi
Amewaasa watumishi wa mahakama hiyo mpya ya Kigamboni kuhakikisha wanatenda haki na kwa wakati na pia waitunze mahakama hiyo ili itumike kwa muda mrefu.
Alibainisha kuwa mfumo wa mahakama wa Tehama utapunguza gharama kwa kuwa utasaidi kesi kuendeshwa wakati shahidi akiwa eneo lingine.
Pia utarahisisha mtu kutumia simu ya kiganjani kupata taarifa za mahakama, kufungua kesi ama kulipa.
Mhandisi wa Jengo hilo, Moses Laurance amesema ujenzi wa jengo hilo umegharimu Sh 594,564,570.40 na ukubwa wa mita za mraba 1168.
Jengo hilo lina kumbi mbili za mahakama, ofisi za mahakimu na watumishi wengine pamoja mahabusu kwa wanaume na wanawake.
Amesema ujenzi huo ulianza Januari 2016 na kwamba utafiti ulikuwa ukiendelea mara kwa mara ujenzi ulisimama kupisha uchambuzi, majadiliano na maamuzi kufanyika
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment