ANC yaadhimisha miaka 100 kuzaliwa Nelson Mandela.....soma habari kamili na matukio360.....#share
Na mashirika ya kimataifa
Chama tawala cha Africa Kusini ANC kimeanza maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka mia moja tangu kuzaliwa kwa rais wa kwanza mweusi nchini humo shujaa, Nelson Mandela.
Kiongozi wa sasa wa ANC ,Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutoa hotuba huko medani mwa Freedom square mjini Cape Town, ambako marehemu Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza alipoachilia huru kutoka gerezani miaka ishirini na nane iliyopita.
Rais Jacob Zuma ambae anakabiliwa na madai chungu nzima ya rushwa amegoma kubanduka huku shinikizo za kumtaka ajiuzulu zikizidi kumzonga .
ANC imetangaza mkutano maalum wa kamati yake kuu ya kitaifa utafanyika Jumatatu kujadili swala hilo.
No comments:
Post a Comment