Barabara Mwigumbi-Maswa kwa kiwango cha lami yakamilika...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu,Dar es salaam
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wakazi wa wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, kuilinda miundombinu ya barabara iliyokamilika kujengwa ili kupunguza gharama za matengenezo ambayo yanaepukika.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu.
Ametoa rai hiyo Wilayani humo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusema kuwa barabara hiyo itawaunganisha wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kukuza uchumi kupitia mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye mikoa hiyo.
"Barabara hii sasa imekamilika ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie kuilinda na kuhakikisha inadumu kwa kipindi kilichokadiriwa", amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa barabara hiyo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi watakaotumia usafiri wa reli ya kisasa pindi utakapokamilika kwani watatoka kwenye mikoa ya jirani kupandia kwenye stesheni ya Malyampaka ambayo iko kwenye barabara hiyo.
Aidha, amewapongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha sehemu ya barabara hiyo na kumuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa miundombinu hiyo italindwa ili idumu muda mrefu.
"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuikamilisha barabara hii kwa kiwango cha lami kwani kwa sasa muda na gharama za usafirishaji wa mazao zitapungua", amesema Dkt. Shekalaghe.
Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema mradi mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 98 na kazi zilizobaki ni kuweka alama za barabarani na ujenzi umezingatia viwango vinavyohitajika.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 imejengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO ambapo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 61.46 na zote zikiwa zimefadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100.

No comments:
Post a Comment