Polisi sita washikiliwa mauaji mwanafunzi NIT....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
KUFUATIA tukio la  kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Akwilini, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo linawashikilia askari polisi sita waliotumia silaha za moto kuwadhibiti waandamanaji katika Jimbo la Kinondoni.

Pia linawashikiria watu 40 kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

Lazaro Mambosasa

Amesema silaha za askari hao zimedhibitiwa kwa uchunguzi na kwamba hatua za kisheria zitachuliwa dhidi ya waliohusika na kifo hicho.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search