Chadema wasitisha kampeni ubunge Kinondoni....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

CHAMA cha Chadema kimesitisha kampeni ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam, Salum Mwalimu ili kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki katika mazishi ya mwanasiasa mkongwe Kingunge Kongambale Mwiru.

Freeman Mbowe

Kingunge anazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. Uamuzi was kusitisha kampeni ulitangazwa jana na mwenyekiti taifa wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano was hadhara uliofanyika katika viwanja vya kwa manyanya Kinondoni.

Mbowe alisema mziba wa Kingunge no mzito kwa kuwa amefanya mengi katika muktaza mzima wa ujenzi wa Tanzania katika uchumi na siasa.

" Katika taifa hili la Tanzania mmoja wa watu waliotumia muda, nguvu na akili kwa ujenzi wa taifa hili ni mzee wetu Kingunge hivyo kesho(leo) tunasitisha kampeni za ubunge ili wananchi washiriki kutoa heshima ya mwisho kwa Mzee Kingunge," alisema Mbowe

Uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Kinondoni unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018. Unatanyika kufuatia aliyeikuwa mbunge wa jimbo hilo Kwa tiketi ya chama cha CUF, Maulid Mtulia kujiuzulu na kujiunga CCM. Na sasa anagombea kupitia CCM

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search