Daraja mto Kilombero lakamilika....soma habari kamili na matukio360....#share
Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
WANANCHI wilayani Ulanga, Malinyi na Kilombero wameishukuru serikali kutimiza ahadi ya kuwajengea daraja la mto
kilombero ambalo limekamilika kwa asilimia mia moja.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua
daraja la mto Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambalo linaunganisha wilaya ya
Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro ambapo mpaka sasa ujenzi wake
umekamilika kwa asilimia 100. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga.
Wakizungumza mbele ya
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji
cha Kivukoni, mkoani Morogoro, wakazi hao wamemueleza kuwa hivi sasa changamoto
zao zimetatuliwa baada ya kukamilika kwa daraja hilo.
“Tunaishukuru Serikali
kwa ujenzi wa daraja hili kwani limekuwa mkombozi kwetu wananchi wa wilaya za
ulanga na kilombero kwani hapo nyuma vifo vingi vimetokea pasipo kutegemewa
wakati tukitumia kivuko kufuata huduma za kijamii wilaya jirani ambapo ndio
kuna huduma zote za muhimu”, amesema Mtalanga.
Aidha waziri Mbarawa ametoa wito kwa wananchi hao kulilinda daraja hilo kwa kutojihusisha na
vitendo vya kuchimba kokoto chini ya daraja, kuiba alama za barabarani na kuacha
kupitisha mifugo juu ya daraja kwani Serikali imetumia gharama kubwa kujenga
daraja hilo na barabara unganishi katika eneo hilo.
Ameongeza kwa sasa
Serikali ipo katika hatua za kujenga
kituo cha polisi katika maeneo hayo ili kimarisha ulinzi na kuhakikisha usalama
unakuwepo kwa saa 24 siku saba kwa wiki.
Naye Meneja wa Wakala
wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro Mhandisi Dorothy Ntenga amemueleza
Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa daraja hilo umejengwa kwa kuzingatia viwango
vilivyowekwa kwenye mkataba na mkandarasi wa kampuni ya M/S China Railway 15
Group Corporation.
Kukamilika kwa ujenzi
wa Daraja la Mto Kilombero umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 ambazo
zimegharamiwa na Serikali na daraja hilo litarahisisha shughuli za usafirishaji
wa mazao, ufugaji na madini katika wilaya hizo na wilaya jirani.
No comments:
Post a Comment