NEC:Maandalizi uchaguzi Kinondoni, Siha yapo vizuri.....soma habari kamili na matukio360...#share



Na Margareth Chambiri, Dar es salaam


ZIKIWA zimebaki siku sita kabla ya uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Siha, Kinondoni na lane kufanyika, Nec imesema maandalizi  ya uchaguzi huo yanaendelea vizuri ikiwamo ufumbuzi wa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe (wa pili kulia) akieleza jambo wakati Tume ilipomtembelea Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni kujua maandalizi ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima amesema hayo mara baada ya mkutano wa watendaji wa tume na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumujuri.

Kailima amesema tume inafuatilia kwa karibu  uchaguzi  unavyoendelea katika maeneo mbalimbali na maafisa wa tume wako maeneo hayo.


"Tumekuja kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ili kupata taarifa juu ya maendeleo ya Maandalizi. Tumekuja hapa kwa sababu  ni rahisi kufika," amesema Kailima


Aidha amewashauri wasimamizi wa uchaguzi kuendelea kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua ya kuelekea Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha vyama vinapata taarifa ya kila hatua.


Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema Tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya Elimu ya Mpiga Kura mfululizo hadi siku ya Uchaguzi, Elimu itakayohusu mada mbalimbali za Uchaguzi zikiwemo Haki na Wajibu wa Mpiga Kura, Wakala wa Vyama vya Siasa na Msimamizi wa Uchaguzi pamoja na taratibu zote za Upigaji Kura.

‘Nawasihi sana watu watembelee Online ya Tume Tv, website ya Tume, kwa jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, facebook na instagram lakini pia App ya Tume, kwa hiyo tumeanza Elimu ya namna hiyo kama eneo la kuelimisha Umma kuelekea tarehe 17 siku ya Kupiga Kura’ amesema Bwana Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na Udiwani katika Kata 8 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi Februari 17, Mwaka 2018.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search