Diamond atoa neno kwa wazazi....soma habari kamili na matukio360....#share
Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam
MWANAMUZIKI Nassib Abdul ' Diamond Platinum' amewashauri wazazi kuweka majivuno yao pembeni wanapokuwa na migogoro na wasimuingize mtoto.
MWANAMUZIKI Nassib Abdul ' Diamond Platinum' amewashauri wazazi kuweka majivuno yao pembeni wanapokuwa na migogoro na wasimuingize mtoto.
Diamond Platinum
Ametoa ushauri huo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kitengo cha watoto ambapo jalada la kesi ya madai ya matunzo ya mtoto lililofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto limefungwa rasmi
Baada ya kutoka mahakamani Diamond amesema walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ili upande wa ustawi na mahakama ziwe sawa ili kisije kikazungumzwa kitu kingine chauongo.
"Nilazima kuweka majivuno pembeni ya matatizo yenu binafsi kwa kuwa mtoto ndiye anaumia, ni lazima muangalie ni namna gani mnatengeneza mazingira mazuri ya kuweza kumlea na kumsaidia mtoto." Amesema Diamond.
Wakili wa Mobeto, Walter Godluck amesema ustawi wa jamii unasaidia katika usuluhishi wa kesi za watoto ambazo zinahusu malezi ambapo baba na mama ukubaliana jinsi wanavyoweza kulea mtoto.
Na kwamba Leo walipeleka ripoti ya usuluhishi mahakamani ambapo kesi ya msingi ya matunzo ya mtoto ilifunguliwa.
Amesema malalamiko waliyoyaleta kuhusu malezi ya mtoto upande wa pili wameridhia na wameona kuna haja ya kuyafanyia kazi na kwamba kiasi cha fedha wamekubaliana ila wamekiweka kifamilia.
Wakili huyo amesema wazazi wamekubali kushughulikia malezi ya mtoto,Diamond yupo tayari kumlea mtoto na yupo tayari kulifanya hilo kwa kadiri inavyowezekana.
Hamisa Mobeto amesema amefurahia maamuzi hayo kwa kuwa upande zote mbili walikaa na wakakubaliana. Ameshukurukuwa kila mtu ameridhika nayo na wamekwisha
.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine alikuwa anaomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto alikuwa anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment