LHRC wamkosoa Paul Makonda.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa
utendaji wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikidai umegubikwa na ukiukwaji utawala wa sheria kwenye utekelezaji wa majukumu
yake.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Felista Mauya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Hatua hii ya LHRC inakuja siku chache baada ya mkuu huyo wa
mkoa kusimamisha utendaji wa mabaraza ya ardhi ya kata kinyume na sheria pamoja
na kudaiwa kuingilia muhimili wa mahakama katika mkutano baina yake na wakazi
wa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Felista Mauya amesema kupitia utendaji kazi wa
serikali kumekuwepo na juhudi mbali mbali za kuboresha ustawi wa maisha ya
wananchi ikiwemo kuwakutanisha wananchi, kuwasikiliza na kuweka mikakati bora
ya kutatua kero zao.
“Hata hivyo ombwe la viongozi wa serikali kutofuata taratibu
na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao limeendelea kuathiri uhalali wa
juhudi hizo,” amesema Mauya.
Ameongeza “Kupitia mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wananchi wa Dar es Salaam uliofanyika Februali 10, 2018, LHRC
kimebaini mapungufu kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa si tu na Paul Makonda pekee bali pia na baadhi ya viongozi wengine wa serikali baadhi ya mapungufu ya
kisheria yanayotokana na mkutano huo ni pamoja na kusimamisha utendaji wa
mabaraza ya ardhi ya kata kinyume na
sheria na kuingilia muhimili wa mahakama."
Mauya amewakumbusha viongozi wa serikali na wanasiasa kuwa
hawana mamlaka ya kisheria kuingilia utendajikazi wa mahakama wala kuelekeza
utendaji wa mahakama badala yake wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu za
kimahakama katika upatikanaji wa haki.
Mapendekezo
Amesema kwa kutambua uwepo wa changamoto za kiuwajibikaji
miongoni mwa watumishi wa umma na changamoto za kiutendaji wa serikali hasa
katika mfumo wa utoaji haki nchini, wametoa mapendekezo saba, miongoni mwa
mapendekezo hayo ni..
Serikali kufuata taratibu za kisehria katika kutatua kero na
changamoto mbali mbali, watendaji wa serikali hasa katika nafasi za kisiasa wanapaswa
kuachakutumia mbinu za kisiasa, badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo
kisheria ili kutatua changamoto na kero za wananchi kwa maendeleo endelevu.
Viongozi wa kisiasa kuacha kutumia mamlaka yao majukwaani
kuwajibisha watumishi wa umma badala yake kufuata taratibu kama zilivyoainishwa
katika sheria ya utumishi wa umma ya 2002.
Watendaji wa serikali kuheshimu muhimili wa mahakama,
viongozi wa serikali wameapa kulinda katiba kupitia Ibara 107 inaipa mahakama mamlaka
ya juu katika kutenda haki.
No comments:
Post a Comment