DSE: Ukubwa mtaji kampuni za ndani wapanda....soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


UKUBWA wa mtaji wa kampuni za ndani Soko la Hisa (DSE), umepanda kwa sh. Bilioni 291 kutoka sh Trilioni 10.1 hadi kufika sh Trilioni 10.4 wiki hii.

Mary Kinabo

Ongezeko hilo ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya VODA kwa asilimia 14, Swissport kwa asilimia 9, Soko la hisa (DSE) kwa asilimia  8 na CRDB 5.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo inasema mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia Februari  2, 2018 yalikuwa sh Bilioni 5.5 ikilinganishwa na mauzo ya sh bilioni 44.6 kwa wiki iliyoishia Januari 26, 2018.


"Idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia iliyoishia Februari 2, 2018 hisa milioni 5.5 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 8 kwa wiki iliyoishia Januari 26, 2018,"amesema


Amesema ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 474 kutoka sh. Trilioni 22.7 wiki iliyopita hadi sh Trilioni 23.2 wiki iliyoishia Februari  2, 2018.


Amesema Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 49 kutoka pointi 2,360 hadi 2,410 pointi hii ikiwa ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Vodacom Tanzania Plc (VODA), Swissport (SWISS), Dar es Salaam Stock  Exchange (DSE) na CRDB Bank Plc (CRDB).


"Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 111 kutoka pointi 3,853 hadi pointi 3,964 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Vodacom Tanzania Plc (VODA), Swissport (SWISS), Dar es Salaam Stock  Exchange (DSE) na CRDB Bank Plc (CRDB).


"Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imepanda kwa pointi 3 kutoka pointi 5,504 hadi pointi 5,507 baada ya hisa za TPCC kupanda kwa asilimia 1.37,"amesema.


Amefafanua kuwa Kiashiria cha huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 37 kutoka pointi 2,555 kadi pointi 2,555 hii imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 8 kutoka sh 1480 hadi sh 1600 na CRDB kwa asilimia 5 kutoka sh 185 hadi sh 195.


Amesema Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda kwa pointi 302 kutoka pointi 2,174 hadi pointi 2,476 imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za VODA kwa asilimia 14 kutoka sh 740 hadi  sh 850.


Akizungumzia mauzo ya hati fungani Mary amesema, Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Februari 2, 2018 yalikuwa sh bilioni 18 kutoka sh Bilioni 23 wiki iliyopita ya Januari 26,2018.



"Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na nne (14) za serikali zenye jumla ya thamani ya sh bilioni 19 kwa jumla ya gharama ya sh  bilioni 18,"amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search