Jinsi Kingunge Kongambale Mwiru atakavyozikwa .....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MWILI wa mwanasiasa mkongwe Kingunge Kongambale Mwiru leo majira ya saa 11  jioni umewasili nyumbani kwake Victoria jijini Dar es salaam ukitokea hospitali ya taifa Muhimbili na kupokelewa kwa uzuni.



Akizungumza msibani hapo mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Omary kimbau amesema taratibu za ibada mila na desturi zitaendelea usiku mzima(mkesha) na atazikwa  Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni.

Hii ndio ratiba kamili;

Jumatatu tarehe 5/2/2018
- Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.

- Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote

- Saa  4:00  asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu 

- Saa 6:00 mwili kuwasili karemjee halll Kwa kuagwa

- Saa 6:00 mchana  9;00 kuaga mwili wa marehemu

- Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini kinondoni

- Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko

- Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani Kwa chakula cha jioni.
waombolezaji wote

1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote

3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli ya Mzee wetu

Matukio360 inatoa pole kwa wote. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search