Kaimu kamishna madini apandishwa kizimbani..soma habari kamili na matukio360...#share..


Na mwandishi wetu, Dar

Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini,Ally Samaje leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka.
Ally Samaje

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,Leonard Swai akimsomea mashtaka mshtakiwa huyo kwa Hakimu Mfawidhi,Victoria Nongwa amedai  mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kati Aprili 9 na Juni  21,2013.


Kwa mujibu wa kesi huyo ya jinai namba 25,2018, Samaje ambaye pia alikuwa Katibu wa bodi ya ushauri wa madini anadaiwa kuwa  wakati akitimiza majukumu yake kwa makusudi alitumia vibaya madaraka kwa kushindwa kuitisha mkutano wa bodi hiyo na kupata ushauri wake.

Kwa kuzingatia maombi ya leseni ya madini namba HQ-P26114 kwa ajili ya  madini  ya Gemstones and associated Minerals  ikiwamo Graphite na Marble katika eneo la Merelani, Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara ambayo iliwasilishwa na kampuni za Tanzaniteone Mining Limited na M/S State Mining Corporation, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 8(4) cha sheria ya madini namba 14 ya 2010 kwa lengo la kuzipatia faida ya eneo la madini la kilometa 7.6 kwa makampuni hayo.

Katika shtaka la pili,Swai alidai kuwa Samaje Aprili 16,2013 alitumia vibaya madaraka yake kwa kutoka maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa leseni na Haki za Madini John Nayopa kuandaa leseni kuchimba madini ya Gemstones ikiwamo Tanzabite,Graphite na Marble bila ya kuzingatia mfumo wa uendeshaji wa taarifa za madini wa Cadastie (MCIMS) wa Wizara ya Nishati na Madini wa eneo la kilometa 7.6 lililopo Mererani Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Kitu ambacho ni kinyume na kifungu cha 49(2)(b) cha sheria ya madini namba 14 ya 2010 na kusababisha kampuni hizo kupata faida ya leseni  za kuchimba madini.

Baada ya kusomewa Mashtaka hayo, Samaje ambaye wanatetewa na Wakili Jema Bilegea alikana na upande wa Mashtaka alidai kuwa upelelezi umekamilika.

Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wenye anuani za kuaminika ambapo kila mdhamini asaini bondi ya Sh 50 milioni.

Pia mshtakiwa huyo asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama, mshtakiwa akitimiza masharti hayo kwa kudhaminiwa na Mhandisi wa Migodi Mwandamizi, Zephania  na Mhasibu Mwandamizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Donald.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 28,2018 ambapo mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali (PH).

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search