Maafisa elimu waonywa kuwashusha madaraja walimu....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu,Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ameonya maofisa elimu kuacha tabia ya
kuwashusha madaraja walimu kwa sababu za matokeo mabaya na kwamba utekelezaji
mikakati ndio chachu katika sekta ya elimu.
"Sio busara kuwaadhibu walimu kutokana na matokeo, njia pekee ni kuweka mikakati kabambe itakayokuwa chachu katika elimu kama nilivyoitisha mkutano wa wadau wa elimu kujalidili changamoto za elimu, kutoka na maazimio, leo yamezaa matunda." amesema
Mkuu wa Mkoa wa mbeya, Amos Makalla (katikati) akitoa tuzo ya kufanya
vizuri katika matokeo ya darasa la saba na nne kwa mwenyekiti wa Halmshauri ya Mbeya Vijiji, Mwalingo Kisemba. Kushoto ni Naibu Spika Dk Tulia Ackson akishuhudia
Naye Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa motisha kwa shule
tano bora zilizofanya vizuri katika mtihani wa Canada la Saba, kidato cha pili na nne
ya Sh milioni 1.2
Ametoa fedha hizo leo katika kikao cha elimu mkoa kilichohitishwa na
mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla na kuhudhuriwa na wakuu wa
wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri, maofisa elimu na wadau
wa elimu kilichoanyika katika ukumbi wa mkapa jijini humo.
Amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa elimu na mkoa kufanya vizuri
kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ameona ni vyema sasa kutoa motisha
ili kuboresha sekta ya elimu mkoani humo
"Nimefurahishwa sana na matokeo ya mkoa kwa kweli wakuu wa wilaya ninaomba
muwape ushirikiano walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri kwani mafanikio ya elimu yanatokana na walimu,wazazi na serikali," amesema Tulia
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment