Maelfu wauaga mwili wa Akwilina....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es salaam
WAZIRI wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako leo ameongoza maelfu ya wakazi wa Dar es salaam kuaga mwili wa marehemu Akwilina Akwilini.
Shughuli hiyo imefanyika katika viwanja vya chuo cha usafirishaji (NIT). Mwili uliwasili majira ya saa sita mchana na ibada ya sala ikiongozwa na kanisa Katoliki ilianza saa saba hadi nane mchana na ulianza kuagwa saa nane hadi majira ya Alasir.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiaga mwili wa Akwilina Akwilini
Picha zaidi;

Wasifu wa marehemu:
Alizaliwa Apri 1, 1996 mkaani Kilimanjaro, wilayani Rombo kijiji Olele-Marangu.
Ni mtoto wa sita kati ya watoto nane wa mzee Akwilini Shirima.
Safari yake ya kielimu alianzia katika shule ya msingi kipogolela darasa la kwanza hadi la saba 2007-2014.
Alijiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari High Land iliyoko mkoani Iringa 2011 hadi 2014.
Alijiunga na kidato cha 5 na 6 Embarai Arusha na baadae Lugalo high School mkoani Iringa 2015 hadi 2017.
Hadi anafariki alikuwa akisoma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) alichojiunga nacho Oktoba 30, 2017 akisomea shahada ya ugavi na usafirishaji na alikuwa mwaka wa kwanza.
Picha zaidi;

No comments:
Post a Comment