Mahakama yampa DPP siku 14....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka ndani ya siku 14 kuja na maamuzi ni lini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ataendelea na kesi ya Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya bilion 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini nchini, Archard Kalugendo na mwenzake.
Archard Kalugendo wa mbele kulia Edward Rweyemamu kushoto wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Hakimu Respicius Mwijage alisema hayo baada ya wakili wa serikali Elizabeth Nkule kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na jalada lipo kwa DPP baada ya kukamilisha maelekezo waliyopewa na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Wakili wa utetezi Ludovic Nickson alidai kuwa jamhuri wanaleta hoja hiyo zaidi ya mara tatu katika tarehe tofauti Novemba 9,2017, Januar 3,2018 na Januari 17,2018.
"Tunachosubiri ni upelelezi kukamilika na kesi kusikilizwa kati ya Kisutu au Mahakama kuu na tunataka kufahamu DPP anachukua muda gani kukamilisha upelelezi"alidai
Alidai kama DPP bado anakazi nyingi awaruhusu watuhumiwa kuomba dhamana wakati anaendelea na shughuli zake ili watuhumiwa wawe nje.
Mshtakiwa mwingine ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu na wote wanakabiliwa na shtaka hilo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi,12,2018 kwaajili ya kutajwa
Inadaiwa kuwa kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini wa Madini waliisababishia hasara Serikali kiasi hicho cha fedha.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.




No comments:
Post a Comment