Majaliwa: Mabalozi tafuteni wawekezaji sekta ya utalii...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi watumieni mbinu za kidiplomasia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameagana Ofisini kwake Dar es salaam na Mabalozi wanao kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizo pangiwa,kulia ni Balozi anaye kwenda Nchini Sweden.Dr Wilbroad Slaa .na kushoto ni Balozi anayekwenda nchini Nigeria Balozi Muhidin Ally  Mboweto

Pia amewataka mabalozi hao wakaimarishe diplomasia kwa lengo la kuzifanya nchi hizo ziendelee kushirikiana na Tanzania katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Ametoa kauli hiyo leo  wakati akizungumza na Balozi Dk. Wilbrod Slaa anayewakilisha Tanzania nchini Sweden na Balozi Muhidin Ally Mboweto anayewakilisha Tazania nchini Nigeria, katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kama uwepo wa fukwe za bahari kuanzia Tanga hadi Mtwara, maziwa na mito, mbuga za wanyama hivyo ni vema wakajielekeza katika kuvutia wawawekezaji kwenye sekta hiyo ili Taifa lipate watalii wengi.

Amesema mbali na kutangaza sekta ya utalii, pia watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
“Tumejiimarisha katika mazao ya chakula na biashara, hivyo tunatakiwa kuwa na uhakika wa masoko kwenye kilimo ili mkulima anapozalisha pamba, tumbaku, kahawa, chai, korosho, dengu pamoja na mazao mengine tuwe na mahali pa kuuza, kwa hiyo washawishini wafanyabiashara kuja kununua.”

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wakawatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio kwenye nchi wanazoiwakilisha ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na wawasisitize wafuate sheria za nchi wanazoishi na wakumbuke nyumbani.

Waziri Mkuu amewasisitiza mabalozi hao kwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa Balozi kwa kuzuia matumizi katika mambo yasiyo ya lazima. “Pia maslahi ya nchi lazima mkayasimamie huko muendako hasa katika masuala ya kiuchumi”

Kwa upande wao mabalozi hao  wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi anaye kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Nchi ya Sweden Balozi Dr. Wilbrodi Slaa . kushoto kwa Waziri Mkuu ni Balozi anyekwenda Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ally  Mboweto.Mabalozi hao walifika ofisi kwa Waziri Mkuu Dar es salaam kwa ajili ya kumuaga .


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search