TFF kuendeleza viwanja tisa nchini...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka 2019 .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahamad alipokuwa nchini kwa ajili ya mkutano wao jijini Dar es Salaam

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA Gianni Infantino alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.

‘’Rais wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia Dola Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo ndiyo zitumike kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja ndio unaosaidia kukuza vipaji vya soka,’’alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya ya pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele kupinga ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.

Pamoja na hayo nae Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika shirikisho hilo FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za maendeleo na kujiendesha tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia uongozi mpya ambao FIFA wameridhika nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia fedha hizo.

‘’Rais wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba tu hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato wa kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi tutakapo pata fedha hizo Shirikisho  litaendeleza baadhi ya miradi ambayo tumekwisha iandaa,’’alisema Bw. Karia.

Pamoja na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliyovamia eneo linalotarajia kujengwa Technical Center  ya mchezo wa soka basi waondoke mara moja kabla hawajachukuliwa hatua.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search