Makonda alia na Jaji mkuu....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba Jaji Mkuu wa Tanzania, kuharakisha na kufanikisha mchakato wa utoaji hukumu kwa lugha ya kiswahili badala ya kingereza.
Pia walimu 2137 wanatarajia kupata malipo ya malimbikizo ya madeni ya sh bil 4.6 huku walimu 5000 wakitarajia kupanda madaraja pamoja na kupandishiwa mshahara mkoani humo.
Paul Makonda
Makonda ameyasema hayo jana baada ya kupokea taarifa ya marejesho ya malalamiko ya wananchi zaidi ya 11000 wa mkoa huo iliyogusa maeneo 12 waliopatiwa msaada wa kisheria kwa siku tano bure kutoka kwa wanasheria zaidi ya 400 na kuvunja mabaraza ya ardhi ya Kata jijini humo kuanzia jana.
Amesema sekta ya ardhi inaongoza kwa migogoro mkoani humo na kwamba wananchi wengi wamekuwa wakikosa haki zao baada ya hukumu hizo kutolewa kwa lugha ya kingereza.
"Hukumu zinatoka kwa kiingereza na sisi hatujui kusoma hapo ndipo tunapopigiwa...kiswahili ndiyo lugha ya taifa nitashangaa sana kwa msisitizo wa kiswahili waziri wa habari anaeneza kiswahili, nitashangaa sana kama mahakama wataendelea kutumia kingereza badala ya kiswahili katika utoaji hukumu, "amesema.
Amefafanua kuwa"Taifa letu lugha yetu ni kiswahili kwanini tunaendelea kutumia lugha ambayo si ya kwetu kwenye mambo ambayo ni ya kwetu?, "amehoji Makonda.
Amesema mlalamikaji na anayelalamikiwa ni waswahili ,hakimu na wa wakili ni waswahili lakini hukumu inatolewa na lugha ya kingereza kwa faida ya nani?
Anaamini Jaji Mkuu ni msikivu na ni Mtanzania atawasaidia kuharakisha mchakato wa kutoa hukumu kwa lugha ya kiswahili ili kila mtu aweze kuelewa hukumu wanazopewa.
Akizungumzia mabaraza ya ardhi ya Kata, Makonda amesema mabaraza hayo yameonekana hayana uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi.
Amesema Mabaraza mengi yamekuwa yakilaumiwa kushindwa kutenda haki kwa wananchi wakati wanapopeleka mashauri yao.
"Kuanzia leo Februari 10 nasimamisha kazi zote za mabaraza ya ardhi ya Kata katika Mkoa wangu na kesi zote zilizopo katika mabaraza yao ziwasilishwe kwa makatibu Tarafa na kuanzia jumatatu nataka makatibu tarafa wapite kwenye mahakama hizo kuchukua kesi pamoja na hukumu zilizopo katika mabaraza hayo,"amesema Makonda.
Kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa wakuu wa idara za ardhi Ilala na Ubungo, Makonda amemuagiza Mkurugenzi wa Mkoa huo, kuwapangia kazi nyingine.
Hatua ya wakuu hao kusimamishwa imekuja baada ya wakuu hao kutakiwa kutaja idadi ya kesi za ardhi waliozipokea katika Idara zao jambo ambalo Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Ubungo, Khamis Songwe kudai Wilaya hiyo haina kesi yoyote ya ardhi ile hali Mkuu wa Mkoa ana takwimu ya kesi zilizopo na kwamba Mkuu wa Idara ya ardhi Ilala kutoa takwimu ambazo si sahihi za kesi wilayani humo.
Kutokana na hali hiyo, Makonda amewaagiza wakurugezi wa Manispaa zote za Mkoa huo kupitia wasifu wa wakuu wao wa Idara kila mmoja na majukumu yake ya kazi kwakuwa kuna wengine hawana sifa ya kazi wanazozifanya
Makonda amemkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala, Salum Hamduni orodha ya majina ya watu wanaodaiwa kuhusika na udalali wa nyumba bila kufuata utaratibu, watendaji wa benki wanaofanya kazi zao bila kufuata utaratibu, watu wanaoghushi hati na kadi za magari na kuuza kwa watu zaida ya mmoja pamoja na watu wanaoghushi nyaraka na kuuza nyumba na maeneo ya watu na kuwakamata ili jumatatu wafikishwe mahakamani.
Pia Makonda amewataka madalali wote wa Mkoa huo wanaohusika kuuza nyumba kwa amri za benki pamoja na mahakama wafike katika ofisi yake siku ya Jumannne wakiwa na nyaraka zao za usajili ili ajiridhishe na kuwafahamu.
amesema benki za Twiga, Kenya Commercial Bank (KCB),bank of Afrika (BOA) zinakazi ya kuwatathmini maofisa mikopo wao kwani wapo wanaouza nyumba za watu pasipo kushirikisha ofisi ya Kata.
"Sitaipa ushirikiano banki yoyote ile inayokwenda kinyume na utaratibu, nilishasema makampuni ya udalali yanayotaka kuuza nyumba kwa amri ya mahakama wapite kwa Mkuu wa wilaya au Katibu Tawala ajiridhishe na nyaraka za mahakama, "amesema.
Makonda pia amewataka wananchi wote waliosikilizwa wafike katika ofisi yake Februari 19 kwaajili ya kuwapatia mawakili ambao watasimamia kesi zao hadi wapate haki zao bure.

No comments:
Post a Comment