Mbowe akanusha Chadema kujitoa katika uchaguzi....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Mwenyekiti taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amekanusha Chadema kujitoa katika uchaguzi wa marudio was ubunge na udiwani utakaofanyika Februari 17, 2018.

Mbowe ameiambia matukio360 kuwa waraka uliotolewa ni propaganda na mchezo mchafu wa kisiasa.

"Ninapozungumza na wewe nipo katika mkutano wa kufunga kampeni. Huo waraka ni propaganda na mchezo mchafu wa kisiasa.Tunashiriki uchaguzi hiyo ni taarifa ya upotoshaji," amesema Mbowe.

Mbowe anatoa kauli hiyo kufuatia kuwapo kwa waraka unaosambaa katika mitandao ya kijamii ikidai  Chadema imejitoa katika uchaguzi

Huu hapa waraka wenye;



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search