Mwanasiasa Tambwe Hizza kuzikwa leo....soma habari kamili na matukio360....#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

MWANASIASA wa siku nyingi, Tambwe Hizza aliyefariki jana alfajiri atazikwa leo
 jijini Dar es salaam katika makaburi ya Chang'ombe wilayani Temeke.


Tambwe Hizza


Mmoja wa wanafamilia, Charles Hizza  ameiambia matukio360 kuwa Hizza alifariki njiani akiwa  ndani ya gari  lake alipokuwa akielekea hospitali kupata matibabu ya ugonjwa wa pumu.

Amesema baada ya kuzidiwa mmoja wa wasamalia wema alimuona na kuingia garini na kumkimbiza hospitali.

Ndugu huyo amesema kabla ya umauti, usiku alisumbuliwa na tatizo Hilo na kulipopambazuka alilazimika kwenda haraka hospitali iliyopo  Mbagala Kizuiani.

"Lakini hakufika, alifariki njiani akiwa katika  gari lake. Ratiba zikikamilika mapema atazikwa leo(Ijumaa) Alasiri katika makaburi ya Chang'ombe Temeke," amesema

Tambwe aliyezaliwa mwaka 1959, ameacha mjane na watoto watatu na mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Kinondoni akiwa ni meneja kampeni msaidizi wa mgombea ubunge, Salum Mwalimu.


Kabla ya kuipigia debe Chadema, Hizza alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa chama cha CUF baadae iling'atuka na kujiunga CCM.

Umaarufu wake uliongezeka mwaka 2005 na 2010 alipogombea ubunge katika jimbo la Temeke jijini Dar es salaam kwa tiketi ya CUF

Kwa mara ya kwanza aliibuka  na kuipigia debe Chadema  kwa mwamvuli wa Ukawa kwenye ufunguzi wa kampeni wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search